Xabi Alonso apasua jipu Chelsea! Awashukia nyota wake
KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amewashukia nyota wake baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Brentford juzi na kukiri kuwa walipoteza “ushindani” katika kipindi cha pili cha mchezo huo mkali. Mwananchi Communications Limited Chelsea ilikumbana na kipigo hicho katika mchezo ambao mabao yote matatu yalifungwa kipindi cha pili, matokeo yaliyofanya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa yanayotarajiwa kuanza keshokutwa. LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amewashukia nyota wake baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Brentford juzi na kukiri kuwa walipoteza “ushindani” katika kipindi cha pili cha mchezo huo mkali. Chelsea ilikumbana na kipigo hicho katika mchezo ambao mabao yote matatu yalifungwa kipindi cha pili, matokeo yaliyofanya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa yanayotarajiwa kuanza keshokutwa. Mbali na kipigo hicho, Chelsea pia ilishindwa kufunga bao kwa mara ya kwanza msimu huu, huku wachezaji wake wakionyesha kiwango cha chini zaidi kwa kipindi chote cha mchezo huo. Alonso amesema timu yake haikuweza kudumisha kiwango na ari ya ushindani kwa dakika zote 90, jambo lililowapa Brentford nafasi ya kutawala kipindi cha pili. “Tulipoteza uthabiti na ushindani katika kipindi cha pili,” amesema Alonso. Kocha huyo amesema Chelsea ilifanya makosa madogo ambayo hatimaye yaliigharimu timu yake, huku akiwapongeza Brentford kwa kutumia vizuri nafasi walizozipata.
Read the original report: mwanaspoti.co.tz →
- Published
- 19 Sep 2026
- Languages
- Kiswahili
- Trending
- brentford vs chelsea